Stori kubwa ya usajili kule EPL ilikuwa Jumatatu hii, sakata na Aubameyang vs Arsenal vs Barcelona. Sasa ni rasmi, yametimia. Auba ni mali halali ya FC Barcelona.
Sakata la Aubameyang na Arsenal limedumu kwa takribani miezi 2 kwenye EPL. Kuvuliwa unahodha, kufanyishwa mazoezi peke yake, kuachwa Uingereza wakati timu ikienda Dubai kuweka kambi n.k hivi vyote ni visa vilivyomuhusu Auba.
Amahakika, kobe akiinama ujue anatunga sheria. Wakati yote yanaendelea, Auba alikuwa kimya. Mikel Arteta akiteka show na kutawala vyombo vya habari mara kwa mara. Januari 31, 2022. Auba akafanya yake, kajibu mashambulizi.
Alianza kwa kuhusishwa na usajili kule Saudi Arabia ambapo iliripotiwa hana mpango wa kwenda falme za kiarabu. Badala yake, atajiunga na timu za Ulaya endapo itatokea anaondoka Arsenal katikati ya msimu huu.

FC Barcelona na Juventus zikatajwa kama timu zinazomuwania Auba. Swali likawa ni, kwa mshahara wake, kuna timu itakayohakikisha haya yametimia? Muda ukaenda haraka, mara paap! Auba yupo uwanja wa ndege jijini Barcelona, Uhispania.
Arsenal wakasema wanashangaa mchezaji huyo kuwa Uhispania wakati ambao, hakukua na makubaliano yeyote kati yao na Barcelona. Ikatoka taarifa kuwa, ameenda kwa sababu zake za kifamilia.
Kabla dirisha la usajili mwezi Januari halijafungwa, ikataarifiwa kuwa, mahusiano ya Aubameyang na Arsenal, yamefikia ukomo baada ya miaka 4. Pande hizi ziliafikiana kuvunja mkataba baina yao na hivyo, Auba akabaki kama mchezaji huru.

Tayari alishaanza mazoezi na kikosi cha FC Barcelona, Arsenal wameshathibitisha kuondoka kwake, Auba ameshathibitisha hilo pamoja na kuwaaga mashabiki wa Arsenal. Barca hawakuwa wamethibitisha hilo.
Sasa yametimia, FC Barcelona wametoa taarifa rasmi ya kumsajili Pierre-Emerick Aubameyang kwa mkataba wa miaka 3 (mpaka 2025).
Taarifa ya Barca imeenda mbali na kusema kuwa, mkataba wao na Auba unakipengele cha kumruhusu kuondoka klabuni hapo ifikapo Juni 30,2023 na, ili kumtoa Auba Camp Nou, anayemuhitaji atapaswa kulipa €100M kufanikisha hilo.
Dakika tano pekee zinakutosha kuwa mmoja wa washindi wa mkwanja mrefu ndani ya kasino pendwa ya meridianbettz katika sloti maridhawa ya KENO, moja ya michezo inayoipa thamani dau lako.


