Mshambuliaji Pierre-Emerick Aubameyang anasema inauma kuondoka Arsenal bila kusema kwaheri baada ya kuondoka katika klabu hiyo kwa makubaliano kabla ya kuhamia Barcelona kwa uhamisho huru.

Taarifa ya Arsenal Jumanne usiku ilithibitisha kuondoka kwa Aubameyang: “Tunamtakia Auba kila la heri kwa kurasa inayofuata katika maisha yake ya soka na tunamshukuru kwa mchango wake kwa klabu.”
Jumanne jioni, Aubameyang alituma ujumbe wa kwaheri kwenye mtandao wa kijamii: “Kwa mashabiki wa Arsenal, asante kwa kuifanya London kuwa nyumbani kwangu na kwa familia yangu kwa miaka minne iliyopita.
“Tulipitia heka heka pamoja na msaada wenu ulimaanisha kila kitu kwangu.
“Kupata nafasi ya kushinda mataji na heshima ya kuwa nahodha wa klabu hii ni jambo ambalo nitaliweka moyoni mwangu milele.
“Siku zote nimekuwa nikizingatia kwa asilimia 100 na kujitolea kufanya kila niwezalo kwa klabu hii ndiyo maana kuondoka bila kuaga inaumiza – lakini hiyo ndiyo soka.
“Nina huzuni sikupata nafasi ya kusaidia wachezaji wenzangu katika wiki chache zilizopita, lakini nina heshima kwa klabu hii na ninawatakia kila la kheri wachezaji na mashabiki wote na miaka mingi yenye mafanikio katika siku zijazo! Love, Auba.”
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 anaondoka Arsenal baada ya miaka minne katika klabu hiyo, baada ya kujiunga akitokea Borussia Dortmund Januari 2018 kwa ada ya £60m ambayo ilikuwa rekodi ya klabu.
Dakika tano pekee zinakutosha kuwa mmoja wa washindi wa mkwanja mrefu ndani ya kasino pendwa ya meridianbettz katika sloti maridhawa ya KENO, moja ya michezo inayoipa thamani dau lako.


