Barcelona Kuuza Mali Zake Ili Kupata Kiasi cha €740 Million

Bodi ya klabu ya Barcelona imeamua kupitisha na kuthibitisha mauzo ya hisa zake za Leseni ya biashara ya klabu na hati miliki za matangazo ya runinga kwenye makubaliano na kampuni ya  CVC, ambapo wanatajia kupata kiasi cha  €740 million ili kuweza kuendesha klabu hiyo.

Mapema leo, bodi ya klabu hiyo ikiongozwa na raisi Joan Laporta, wamekutana La Jonquera kwa ajiri ya kuzungumzia hatua inayofuata ili kuweza kuinusuru klabu hiyo kutoka kwenye kifungo cha matatizo ya kifedha.

Barcelona

Kwa sasa Barcelona hiawezi kufanya usajiri wa mchezaji yoyote mpya au kumsanisha mchezaji aliyemaliza muda wake kwenye klabu hiyo, kutokana na matatizo ya kiuchumi waliyonayo. Ambapo sasa wamepanga kufanikisha deal mbazo zitawaingizia kiasi kikubwa cha fedha kwenye klabu hiyo.

Kwa taarifa iliyopo sasa, bodi imeamua kuuza hisa zake asilimia 45 kwa BLM, ambazo zina thamani inayokaribia €200 million kutoka kwa washirika wanaounda Fanatics and Investindustrial.

Pia Barcelona wamekuwa wakifanyia kazi deal hili kwa muda kidogo sasa, ambapo sasa hivi inaoneka kuwa mpango huo unakwenda kupita, baada ya kuwekwa pembeni kwa ajiri ya kuthibitishwa na wajumbe. Ingawa, deal hilo linaonekana kuwa linakwenda kukamilika kabla ya June 30, lakini klabu inanjia nyingine ya kupata pesa iliijikwamua kwenye tatizo hilo.

Barcelona

Barcelona pia wamepnga kuingiza kiasi cha  €540milion kwenye uwekezaji wao, kwa kuuza hatimiliki za matangazo ya runinga kwa asilimia 25% kwa kampuni moja au zaidi.

La Liga inawapigia upatu CVC kwenye deal ambalo inaonekana kufanikiwa, na Barcelona wataidhinishia kiasi cha €270 million kama mkopo usio na riba, huku kukiwa na sheria ya mabadiliko ya 8.2% kutoka kwenye faida watakayoipata kwenye hatimiliki ya matangazo ya sauti kwa misimu 50 ijayo.

Licha ya hayo, Barcelona wamekuwa kwenye mapatano na kampuni ya Goldman Sachs ili kupata kiasi cha  €270 million kutoka kwenye haki za matangazo, japokuwa maelezo ya mpango huo bado hayako wazi kwa sasa.

Barclona wamepanga kufanya kikao mwezi june 16, ili kuweza kupiga kura mapendekezo hayo mawili yaliotolewa na bodi kupitishwa na kuanza kifanyiwa kazi.


SHINDA SAMSUNG A32 NA AVIATOR

SHINDA Samsung A32 ukiwa na mchezo wa Aviator kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet! Kwea pipa ukusanye zawadi zako pamoja na ushindi mnono wa mkwanja!

kasa wa njano, Kasa wa Njano Awapa Ubingwa wa CL Liverpool., Meridianbet

SOMA ZAIDI HAPA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.