Raisi wa klabu ya Barcelona Joan Laporta amemshtumu raisi wa La Liga Javier Tebas kuhusu kauli yake inayohusu uwezo wa klabu hiyo kusajiri wachezaji.
Javier Tebas akifanya mahojiano na MARCA, alisema kuwa Barcelona haina nafasi ya kuweza kumsajiri mshambuliaji wa klabu ya Bayern Munich Robert Lewandowski kwenye majira ya kiangazi, kuwa ni lazima wauze wachezaji kwanza kabla ya kufikilia kuingiza wachezaji.
“Barcelona wnajua nini wanapaswa kufanya. Wanajua vizuri kanuni zetu za kusimamia uchumi na maswala yao ya kifedha. Sheria zipo kwa ajiri ya kuepuka matatizo ya kiuchumi. Sijui kama wata muuza De jong , Pedri au Pepito Perez,”
Wanajua nini wanapaswa kufanya, Uza mali na upate zaidi , hichi ndicho wanapaswa kufanya, Barcelona wamepata hasara nyingi sana kwenye mwaka wa mwisho wa kodi, ambapo ilikuwa inawezekana kuepukika.
Kama ilivyo kwa Real Madrid wana nafasi kubwa ya wazi, Barcelona hawana. Kwa sasa hawawezi kumsajiri Lewandowski.
Joan Laporta amemjibu kwenye waraka huo na kusema kuwa, “Tebas anajaribu kuichafua klabu hiyi na kumwambia ajizuie kuisema klabu ya Barcelona kwenye uhamisho.
“Nakuomba ujizuie kuizungumzia kuhusu uhamisho ambao klabu ya Barca inayoweza kufanya,” Joan Laporta alisema, kabla ya kuongezea, “kama Tebas anafanya hili kwa makusudi, haikubaliki kwetu, na kama hakuzamilia, yeye ni mzungumzaji na anapenda kutafuta sifa.
“Kwenye waraka wa Tebas, inaonekaza dhahiri kuwa alikuwa ana nia ya kiharibu sifa ya Barcelona.” Joan Laporta aliongezea.
SHINDA Samsung A32 ukiwa na mchezo wa Aviator kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet! Kwea pipa ukusanye zawadi zako pamoja na ushindi mnono wa mkwanja!