Klabu ya AC milan inakaribia kununuliwa na kampuni ya uwekezaji kutoka marekani ya RedBird kutoka kwa hedge fund Elliott, chanzo cha habari ni kutoka nchini Italia waliwaambia Reuters.
Shirika la habari nchini Italia ANSA walitoa taarifa mapema kwamba mauzo yamekamilika lakini chanzo kilisema kuwa pande hizo mbili bado zinafanyia kazi dili hilo, pia tangazo rasmi halitarajiwi kutoka leo.

RedBird wamekataa kuzungumzia chochote kuhusu dili hili kama limekamilika.
Asset manager Investcorp alikuwa ni mmoja ya kampuni iliyokuwa inataka kuinunua mabingwa hao mara saba wa ulaya AC Milan mapema mwezi huu lakini hawakuweza kukubaliana kwenye baadhi ya masharti, na kuwafanya Redbird kuingia kwenye kinyanganyiro.
Gazeti la Italia Il Sole 24 Ore imeripotiwa mapema mwezi huu kwamba Redbird wanakaribia kukamilisha dili hilo lenye thamani ya 1.3billion euros kununua klabu ya AC milan.
AC Milan ni moja ya klabu ambayo ilikuwa inamilikuwa na waziri mkuu wa zamani wa Italia Silvio Berlusconi.
RedBird, tayari wameshafanya uwekezaji katika Fenway Sports Group, kampuni abayo inamiliki klabu ya Liverpool inayodhiriki ligi kuu ya Uingereza na klabu ya baseball Red Sox pia wanamiliki hisa kwenye klabu ya Toulouse ambayo iko nchini Ufaransa.
AC Milan wamepata ubingwa wao wa 19 kwenye ligi kuu ya Serie A siku ya mwisho ya msimu ikiwa ni kombe lao la kwanza ndani ya miaka 11.
SHINDA Samsung A32 ukiwa na mchezo wa Aviator kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet! Kwea pipa ukusanye zawadi zako pamoja na ushindi mnono wa mkwanja!


