Tetesi zinasema, Manchester United wanafikiria kumnunua kiungo wa kati wa Chelsea na England Mason, Mount, 23, ambaye bado hajasaini mkataba mpya Stamford Bridge.

Liverpool wanamfuatilia mshambuliaji wa Rennes Mfaransa Martin Terrier, 25, kama mbadala wa Sadio Mane, iwapo mchezaji huyo wa kimataifa wa Senegal, 30, ataondoka Anfield.

Tetesi zinasema, Meneja wa Barcelona Xavi amefanya mazungumzo na kiungo wa kati wa Wolves na Ureno Ruben Neves, 25, kuangalia uwezekano wa kumsajili.

 

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

Tetesi zinasema, Juventus wanaendelea kumtaka beki wa Manchester City Mhispania Aymeric Laporte, 28.

Tetesi zinasema, Beki wa kushoto wa Manchester City wa Ukraine Oleksandr Zinchenko, 25, anavivutiwa vilabu vya Everton na Newcastle.

West Ham wanakaribia kukamilisha mpango wa kumsajili beki wa Rennes Nayef Aguerd. The Hammers pia walijaribu kumsajili mchezaji huyo wa Morocco mwenye umri wa miaka 26 msimu uliopita wa joto.

Tetesi zinasema, Chelsea wamefufua nia yao ya kumnunua beki wa pembeni wa Barcelona na Marekani mwenye umri wa miaka 21,Sergino Dest.

 

Sergino Dest Barcelona
Sergino Dest, Barcelona

Inter Milan wanatarajiwa kufanya mazungumzo na mwanasheria wa mshambuliaji wa Chelsea Romelu Lukaku, 29, kuangalia namna mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji anavyoweza kurejea Serie A

Leeds United wanakabiliwa na vita ya fedha ya pauni milioni 10 dhdi ya klabu ya Bundesliga Borussia Dortmund ili kumsajili beki wa kulia wa kimataifa wa Denmark Rasmus Kristensen, 24, kutoka Red Bull Salzburg.

Barcelona wamemuweka sokoni kwa mkopo mlinzi wa kimataifa wa Ufaransa Clement Lenglet, 26, huku vilabu kadhaa vya ligi kuu England vikionyesha nia ya kumtaka.


SHINDA SAMSUNG A32 NA AVIATOR

SHINDA Samsung A32 ukiwa na mchezo wa Aviator kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet! Kwea pipa ukusanye zawadi zako pamoja na ushindi mnono wa mkwanja!

kasa wa njano, Kasa wa Njano Awapa Ubingwa wa CL Liverpool., Meridianbet

SOMA ZAIDI HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa