Dani Alves: Mlinzi wa Zamani Barcelona Afungwa Mahabusu kwa Makosa ya Ngono

Mlinzi wa Brazil Dani Alves anashikiliwa kwa muda gerezani huku akisubiri uchunguzi kuhusiana na madai ya unyanyasaji wa kingono yanayomkabili. Meridianbet wanatoa ODDS kubwa kwenye mechi zote. Bashiri hapa.

 

Dani Alves

Mlinzi huyo wa Barcelona, mwenye umri wa miaka 39, kwa mujibu wa BBC anadaiwa kumyanyasa mwanamke kwa kumgusa sehemu ya mwili wake kwa namna isiyofaa walipokuwa katika ukumbi wa starehe wa usiku mjini Barcelona mwezi Disemba.

Dani Alves, ambaye alikana madai hayo, alipelekwa mahabusu na kuhojiwa na jaji mjini Barcelona Ijumaa.

Klabu yake, ya Mexico Pumas UNAM, ilikatisha mara moja mkataba wa Alves, kufuatia madai hayo. Beti na Meridianbet mechi za ligi zote, odds ni kubwa sana, Usikose hii!!

“Klabu ilirejelea kusema kuwa haiwezi kuvumilia vitendo vya mmoja wao yeyote, hata awe nani, ambavyo vinakwenda kinyume na maadili ya klabu ,” alisema Rais wa mchezo wa klabu ya Pumas, Leopoldo Silva.

“Hatuwezi kuruhusu mwenendo wa mtu mmoja kuharibu falsafa ya kazi yetu, ambayo imekuwa ya mfano wa kuigwa katika kipindi chote cha historia ya klabu.”

Dani Alves aliiichezea Barcelona mara 408 na pia alikuwa sehemu ya kikosi cha Brazil katika Kombe la Dunia la 2022. Ukiwa na meridianbet unaweza kubashiri mubashara, tembelea maduka ya meridianbet uweze kubashiri.

Polisi wa eneo hilo Mossos d’Esquadra amethibitisha taarifa ya kukamatwa na kufungwa kwa Dani Alves kwa mashirika ya habari ya Reuters na AFP. Odds kubwa za soka unazipata Meridianbet.

Acha ujumbe