Kiungo wa Klabu ya Simba raia wa DR Congo, Fabrice Ngoma amerejea ndani ya timu na kuipa matumaini makubwa timu hiyo, katika michezo ijayo ya Ligi Kuu Bara ukiwemo dhidi ya Azam FC Utakaochezwa leo CCM Kirumba, Mwanza. Beti na Meridianbet kwa odds kubwa na machaguo kibao, pia unaweza kubashiri mubashara.
Kiungo huyo aliukosa mchezo wa ligi dhidi ya Mashujaa FC sambamba na ule wa jana mbele ya Tabora United kutokana na kuwepo nyumbani kwao DR Congo.
Fabrice Ngoma anaunda safu ya kiungo ukabaji inayochezwa na Babacar Sarr, Sadio Kanoute, Mzamiru Yassin na Abdallah Khamis.
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally alisema kuwa kiungo huyo juzi Jumatatu alianza mazoezi mepesi akitokea kwao DR Congo alipokwenda kumaliza matatizo ya kifamilia baada ya uongozi kutoa baraka za kwenda huko.
Ahmed alisema kuwa kiungo huyo alianza kwa mazoezi mepesi kuhakikisha anakuwa fiti na tayari kwa ajili ya michezo ijayo ya ligi ukiwemo dhidi ya Azam FC watakaoucheza Ijumaa ya leo kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza. Odds kubwa, kasino ya mtandaoni na michezo ya sloti ni njia rahisi ya kukupa mtonyo mrefu. Ingia mchezoni hapa.
Aliongeza kuwa kurejea kwa Ngoma kutaimarisha safu yao ya kiungo katika kujiandaa mchezo dhidi ya Azam, ambao anaamini ni mgumu kwao kutokana na upinzani unaokuwepo wanapokutana.
“Jana (juzi) jioni Ngoma alianza mazoezi mepesi ya binafsi hapa Tabora kujiandaa na michezo ijayo ya ligi na kimataifa, baada ya kurejea nchini akitokea kwao DR Congo alipokwenda kumaliza matatizo ya kifamilia.
“Fabrice Ngoma alikosekana katika michezo miwili, lakini katika michezo ijayo ya ligi, anatarajiwa kuwepo kuipambania timu yake ukiwemo huu wa Dabi ya Mzizima dhidi ya Azam.
“Uwepo wake katika mchezo huu dhidi ya Azam, ataimarisha safu ya kiungo ukabaji, akisaidiana na wenzake akina Sarr, Kanoute, Mzamiru na wengine kuhakikisha tunaimilika safu ya kiungo,” alisema Ahmed.
Jisajili na Meridianbet upate bonasi kibao na odds kubwa za ubashiri kwa machaguo kibao.