Graham Potter Kurejea Nice ya Ufaransa

POTTER

Aliyewahi kuwa kocha mkuu wa Chelsea Graham Potter anaripotiwa kurejea kwenye uongozi katika klabu ya Nice ya Ligue 1. Pata odds kubwa kutoka Meridianbet kwa mechi za ligi mbalimbali.

Potter 48 alitimuliwa Chelsea mwezi Aprili baada ya kuifundisha kwa miezi saba pekee.

Siku kadhaa baadaye aliteuliwa kama mgombeaji wa nafasi iliyo wazi ya Leicester baada ya kufukuzwa kwa Brendan Rodgers.

Lakini alijiondoa kwenye kinyang’anyiro cha kuwania nafasi hiyo huku akitazama kwa muda mbali na soka. Ukiwa na meridianbet unapata odds kubwa, kasino ya mtandaoni na michezo ya sloti.

Lakini kwa mujibu wa L’Equipe, Potter anaripotiwa kurejea katika mchezo huo wiki saba tu baada ya kuondolewa na Chelsea.

Klabu ya Nice ya Ufaransa, ambayo inajivunia nyota wa zamani wa Ligi Kuu kama vile Aaron Ramsey, Ross Barkley na Kasper Schmeichel, inasemekana kumtaka kocha huyo wa zamani wa Brighton.

Kocha wa zamani wa Borussia Dortmund Lucien Favre aliteuliwa msimu wa joto lakini alidumu kwa miezi mitano tu kabla ya kutimuliwa Januari. Beti na Meridianbet kwa odds kubwa na machaguo kibao, pia unaweza kubashiri mubashara.

Didier Digard amechukua uongozi wa muda hadi mwisho wa msimu – na wanashika nafasi ya tisa kwenye msimamo huku kukiwa na michezo miwili iliyosalia.

Lakini wanawinda kocha mkuu wa kudumu na Potter anaweza kuwa mtu wao.

Nice inamilikiwa na bilionea wa Uingereza Sir Jim Ratcliffe – ambaye ni mmoja wa wazabuni wanaoongoza katika kinyang’anyiro cha kuinunua Manchester United. Tembelea duka la ubashiri-Meridianbet kutandika jamvi lako kwa odds kubwa.

Acha ujumbe