Mtoto ni Muuaji: Wakala wa Kiungo Mpya wa Man Utd Marcel Sabitzer

‘Mtoto ni muuaji’: Wakala wa Marcel Sabitzer afichua jinsi kiungo huyo ‘asivyopendeza’ wakati anacheza baada ya kukamilisha uhamisho wa mkopo kwenda Man United kutoka Bayern Munich. Meridianbet wanatoa ODDS kubwa kwenye mechi zote. Bashiri hapa.

 

sabitzer

Wakala wa Marcel Sabitzer amefichua hayo baada ya kukamilisha uhamisho wa mkopo kwenda Manchester United kutoka Bayern Munich siku ya mwisho ya uhamisho.

Sabitzer alithibitishwa kujiunga na Mashetani Wekundu mida ya jioni kabisa baada ya Christian Eriksen kuondolewa kwa miezi mitatu ijayo. Beti na Meridianbet mechi za ligi zote, odds ni kubwa sana, Usikose hii!!.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Austria alisafiri kwa ndege hadi Manchester usiku wa kuamkia jana kukamilisha uhamisho wake wa mkopo wa msimu mzima kwenda Old Trafford, huku Red Devils wakiwasilisha karatasi ya makubaliano kabla ya tarehe ya mwisho ya saa 11 jioni.

Wakala wa kiungo huyo Roger Wittmann, hata hivyo, amefunguka kuhusu mawazo ya Sabitzer ya kushinda na jinsi anavyotaka kucheza mara kwa mara baada ya kuwa nje ya Bayern msimu huu.

 

-sabitzer-Manchester United

“[Yeye] ndiye mtu asiyependeza zaidi kuwa karibu naye wakati hachezi,” Wittmann alisema kupitia Goal.

“Anachukia anaposhindwa. Hiyo ndiyo msingi kulingana na tabia, mtoto ni muuaji. Hivyo ndivyo wachezaji wanaotaka kushinda kila mara wanavyoonekana.”

Sabitzer hajaanza mchezo kwa wababe hao wa Bundesliga tangu kabla ya Kombe la Dunia mapema Novemba – wakati wa ushindi wao wa 2-0 wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Inter Milan.

Sabitzer anaongeza ubora kwenye safu ya kiungo ya Erik ten Hag sambamba na mastaa kama Casemiro, Scott McTominay, Fred, na Bruno Fernandes. Ukiwa na meridianbet unaweza kubashiri mubashara, tembelea maduka ya meridianbet uweze kubashiri.

Amecheza mara 54 tangu atue Bayern mwaka 2021, akifunga mara mbili, lakini amekuwa na wakati mgumu kupachika soka la kawaida katika kikosi cha kwanza.

Sabitzer alianza mara nane pekee katika Bundesliga msimu uliopita, akitokea benchi mara 17 – akifunga mara moja na kutoa asisti moja.

Alijitengenezea jina katika RB Leipzig na maonyesho ya kuvutia kati ya 2014 na 2021.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 aliichezea Leipzig mara 229 kwa jumla, akifunga mabao 52 kabla ya kupata uhamisho wa £14m kwenda Bayern. Odds kubwa za soka unazipata Meridianbet.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.