Manchester City wameshtakiwa na Premier League kwa kukiuka sheria za kifedha zaidi ya mara 100 kwenye misimu tisa iliyopita. Odds kubwa za soka unazipata Meridianbet.

Mashtaka dhidi ya mabingwa hao watetezi yanahusiana na taarifa za fedha kuhusu mapato, maelezo ya malipo ya meneja na wachezaji, kanuni za UEFA, faida na uendelevu na ushirikiano na uchunguzi wa Ligi Kuu.
Taarifa kutoka EPL ilisema ukiukaji unaodaiwa ulifanyika kuanzia Septemba 2009 hadi msimu wa 2017-18 na sasa utatumwa kwa tume huru. Manchester City pia wanakabiliwa na mashtaka ya kushindwa kutoa ushirikiano wa uchunguzi ulioanza Desemba 2018.
Inaongeza kuwa klabu hiyo inadaiwa kukiuka kanuni za ligi zinazohitaji kutolewa kwa nia njema kabisa kuhusu taarifa sahihi za kifedha zinazotoa mtazamo wa kweli na wa haki wa hali ya kifedha ya klabu. Ukiwa na meridianbet unaweza kubashiri mubashara, tembelea maduka ya meridianbet uweze kubashiri.
Iwapo Manchester City watapatikana na hatia, watakabiliwa na vikwazo vingi ikiwa ni pamoja na kukatwa pointi au hata kushushwa daraja, ingawa inaweza kuchukua miaka kufikia tamati wa maamuzi hayo.
Klabu bado haijatoa maoni yoyote kuhusiana na taarifa hiyo kutoka Premier League. Beti na Meridianbet mechi za ligi zote, odds ni kubwa sana, Usikose hii!!.
Kati ya tarehe zilizotajwa, Man City ilishinda mataji matatu ya Ligi Kuu, Kombe la FA na Vikombe vitatu vya Carabao.
Premier League ilisema kuwa “Kwa mujibu wa Kanuni ya EPL W.82.1, Ligi Kuu inathibitisha kwamba leo imeelekeza madai ya ukiukaji wa Kanuni za Ligi Kuu na Klabu ya Soka ya Manchester City kwenye Tume.”
Manchester City wamekanusha vikali ukiukaji wowote wa sheria za kifedha lakini uchunguzi ulianza Desemba 2018 baada ya tovuti ya Ujerumani Der Spiegel kuchapisha nyaraka hizo ilizozipata kutoka kwa mdukuzi Mreno Rui Pinto.
Ilidaiwa kuwa City ilizidisha mapato ya udhamini kwa pesa zilizolipwa kutoka kwa wamiliki wa klabu hiyo badala ya wafadhili wanaohusishwa na Abu Dhabi. Pata Odds za soka ukiwa na Meridianbet.

Mshahara wa Roberto Mancini ulisemekana kuongezeka maradufu kupitia mkataba wa siri na klabu ya Abu Dhabi alipokuwa Man City, huku pia wakidaiwa kukiuka sheria za kuwakaribia wachezaji chipukizi. Meridianbet wanatoa ODDS kubwa na zawadi ya ukaribisho ukijiunga. Bashiri hapa.

