Rashford Mchezaji Bora wa Mwezi Januari Epl

Mshambuliaji wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya Uingereza Marcus Rashford amefanikiwa kua mchezaji bora wa mwezi Januari ndani ya ligi kuu ya Uingereza.

Marcus Rashford amekua kwenye kiwango bora tangu atoke kwenye michuano ya kombe la dunia nchini Qatar, Mchezaji huyo amekua na mfululizo wa kufunga kwenye michezo saba mfululizo kuanzia mwezi Disemba mpaka ndani ya mwezi Januari.RashfordMshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uingereza amekua kwenye ubora wa hali ya juu jambo lililomfanya kuweza kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi wa ligi kuu ya Uingereza, Mchezaji huyo amefanikiwa kuwashinda nyota kadhaa aliokua akigombania nao tuzo hiyo ikiwemo nyota mwenzake wa kimatifa wa Uingereza Bukayo Saka.

Marcus Rashford anafanikiwa kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi kwa mara ya pili msimu huu huku akiwa mchezaji wa kwanza kufanya hivo msimu huu, Mchezaji huyo alifanikiwa kushinda tuzo ya mchezaji bora wa ligi kuu ya Uingereza mwezi wa tisa mwaka jana na mwezi Januari mwaka huu.RashfordMshambuliaji Marcus Rashford ameweka rekodi pia kwenye maisha yake kwani ameweza kushinda tuzo hiyo mara moja tu kwenye misimu saba aliyofanikiwa kucheza ligi hiyo, Lakini msimu huu tayari ameshashinda tuzo hiyo mara mbili ikiwa msimu bado haujamalizika hivo inawezekana akashinda tuzo hiyo kwa mara nyingine.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.