Mamlaka ya Ligi kuu ya Uingereza imepitisha utaratibu mzuri wa kuwaruhusu wachezaji wenye imani ya Kiislamu kufturu katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhan, wakati wa michezo yote ya jioni ambapo Mohamed Salah na Riyad Mahrez ni miongoni mwa nyota wa Premier League ambao ni waislamu.

Odds kubwa za soka unazipata Meridianbet Kasino ya mtandaoni, sloti, Poker, Aviator na Roulette- Chagua Tukupe.
Mwezi mtukufu wa Ramadhan ulianza Jumatano, Machi 22 na utadumu kwa mwezi mmoja, huku wachezaji Waislamu wakijizuia kula na kunywa wakati wa mchana.
Kwa mujibu wa Sky Sports ilifichua Jumapili kwamba wasimamizi wa mechi katika Ligi Kuu na EFL wamepewa mwongozo wa kuwaruhusu wachezaji kufuturu wakati wa michezo.
Jua linapozama wataruhusu kusitishwa kwa mchezo na kisha kuwaruhusu wachezaji kufungulia wakiwa pembeni ya uwanja.
Viongozi hao pia wamehimizwa kubaini wachezaji ambao wako kwenye mfungo kabla ya mchezo ili kukubaliana muda uliokadiriwa wa kusitisha kucheza. Beti na Meridianbet mechi za ligi zote, odds ni kubwa sana, usikose pia Kasino ya mtandaoni ya Meridianbet yenye michezo rahisi ya sloti kama Poker, Aviator, Roulette.
Ramadhani ni mwezi wa tisa wa kalenda ya Kiislamu na inazingatiwa na Waislamu duniani kote kama wakati wa kufunga, kufanya ibada, kutoa swadaka na Zaka.
Nyota wa Liverpool, Mohamed Salah, winga wa Man City Mahrez na N’Golo Kante wa Chelsea ni miongoni mwa wachezaji wengi ambao ni waumini wa dini ya Kiislamu nchini Uingereza.

Hii ina maana kwamba idadi kubwa ya michezo katika mwezi ujao itakuwa na mapumziko ya kucheza yaliyopangwa ili wachezaji wapate chakula na vinywaji.
Abdoulaye Doucoure wa Everton amekuwa akizungumza na BBC kuhusu jinsi anahisi ligi hiyo inasaidia kuwaunga mkono wachezaji Waislamu. Ukiwa na meridianbet unaweza kubashiri mubashara, tembelea maduka ya meridianbet uweze kucheza michezo ya sloti na kasino ya mtandaoni.
Alisema: “Tunajisikia kujiamini sana hapa, tunakubalika sana na kila kitu kiko sawa kwa Waislamu kufurahia.
“Kwenye Ligi Kuu, uko huru kufanya chochote kinachokufaa. Hawatafanya chochote kinyume na imani yako na hii ni nzuri.
“Mimi hufunga kila siku, sikosi siku yoyote. Imekuwa kawaida na rahisi sana kwangu.
“Mazoezi bado ni yale yale wakati wa Ramadhani, lakini tunapoenda (kwenye mechi za ugenini), tunaweza kuhitaji kula baadaye kuliko wengine, kwa hivyo mpishi anatuandalia chakula, akihakikisha kila kitu kiko sawa kama nyumbani. Tunapata chakula cha halali kwa hivyo hakuna shida.
Mnamo 2021, Wesley Fofana na Cheikhou Kouyate waliruhusiwa kufuturu wakati wa mechi kati ya Leicester na Crystal Palace. Pata Odds za soka ukiwa na Meridianbet na kasino ya mtandaoni.

