Tuchel: Nilishangazwa Bayern Kunihitaji Wakati Huu

Kocha wa klabu ya Bayern Munich Thomas Tuchel amesema alishangazwa na mabosi wa klabu ya Bayern kumtafuta kipindi hichi kwakua hakua anawaza kufanya kazi majira haya na alipanga kurudi kazini majira ya joto.

Kocha Tuchel anasema mipango yake kurudi kufundisha alipanga kurudi majira ya kiangazi hata alipopokea simu ya mabosi wa klabu ya Fc Bayern Munich alifikiri ni mazungumzo kwajili ya majira ya kiangazi lakini haikua hivo na walifikia hatua ya kumpatia timu kipindi hichi.TuchelKocha huyo anasema hakua na mbinu zozote kwakua hakua na mipango ya kufanya kazi huku akisema kulikua na vilabu kadhaa viliulizia huduma yake, Lakini akili yake aliiweka kufikiria zaidi majira ya kiangazi ni wazi Bayern wamefanikiwa kubadili akili yake.

Kocha Tuchel licha kuweka wazi hakua tayari kuanza kufundisha kipindi hichi lakini jana alifanikiwa kuanza vizuri katika mchezo wake wa kwanza klabuni hapo, Hiyo ni baada ya kupata ushindi mnono dhidi ya Borussia Dortmund wa mabao 4-2 na kufanikiwa akuirudisha Bayern Munich kileleni.TuchelBaada ya Tuchel kukabidhiwa timu hiyo kutoka kwa Julian Nagelsman matarajio ni makubwa kwa kocha huyo wa zamani wa vilabu vya Chelsea, Dortmund, na PSG matumaini makubwa yamewekwa kwa kocha huyo haswa kwenye ligi ya mabingwa ulaya ambapo kocha huyo ameshinda taji hilo mwaka 2021.

 

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.