Tuchel Aanza Kibabe Bayern Munich

Kocha wa zamani wa klabu ya Chelsea Thomas Tuchel ambaye anaifundisha klabu ya Bayern Munich kwasasa amefanikiwa kuanza vizuri ndani ya timu hiyo baada ya kuifunga klabu yake ya zamani ya Borussia Dortmund katika mchezo wa ligi kuu ya Ujerumani.

Bayern Munich wamefanikiwa kuifurumusha klabu ya Borussia Dortmund kwa mabao 4-2 katika mchezo wa ligi kuu nchini humo, Huku Tuchel akiiongoza timu hiyo kwa mara ya kwanza.TuchelKlabu ya Borussia Dortmund ambao walikua vinara wa ligi kuu ya Ujerumani Bundesliga wakiwa kileleni kwa alama 53, Sasa wameshushwa rasmi na Bayern Munich wamerudi kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo baada ya matokeo ya mchezo wa leo uliopigwa katika dimba la Allianz Arena.

Kocha Tuchel baada ya kuanza vizuri katika mchezo wake wa kwanza ndani Bayern Munich sasa anakabiliwa na mtihani mzito mbele yake kwenye michuano ya ligi ya mabingwa ulaya dhidi ya klabu ya Manchester City mchezo unaotarajiwa kua mkali sana baina ya vilabu hivo.TuchelMchezo huo utakua ni kama wa kisasi baina ya Tuchel na Guardiola kwani kocha huyo alimfunga Guardiola kwenye fainali ya ligi ya mabingwa ulaya mwaka 2021, Vilevile Guardiola atakua anakutana na waajiri wake wa zamani hivo ni mchezo mkali wenye historia ya kusisimua kwa pande zote mbili.

 

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.