Simba sports club tayari imeshatua nchini Malawi asubuhi ya leo tayari ya kwa mchezo wa ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya Nyassa Big Bullets.

Klabu ya Simba baada ya kupata matokeo yasiyoridhisha kwenye mchezo uliopigwa jana katika uwanja wa Benjamin Mkapa wakipata suluhu dhidi ya KMC timu ya manispaa ya Kinondoni.

Simba wanatarajia kucheza mchezo wao wa hatua za awali siku ya jumamosi dhidi ya Nyassa big bullets ya Malawi katika mchezo wa kwanza ambapo mchezo wa pili utapigwa katika dimba la Benjamin Mkapa Simba watakua wenyeji wa mchezo huo.

simbaTaarifa ya kushtua ilitoka usiku wa jana baada ya klabu hiyo kumteua kocha wa Coastal Union ya Tanga Juma Mgunda kua kocha mkuu wa muda wa klabu hiyo baada ya timu kua chini ya Suleimani Matola toka kuondoka kwa kocha mkuu wa klabu hiyo.

Klabu ya Simba ililazimika kumtetua Mgunda kukaimu nafasi ya kocha mkuu kwakua ana vigezo vya kukaa kwenye benchi la ufundi kama kocha mkuu kwenye michuano ya Caf kitu ambacho kisingewezekana kwa Matola ndipo Simba wakalazimika kufanya maamuzi hayo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa