Kocha mkuu wa Bayern Munchen Julian Nagelsman amesema kuwa timu yake ilistahili ushindi kabisa hapo jana dhidi Intermillan. Mchezo ambao Bayern alikuwa mgeni wa Intermillan katika uwanja wa San Siro ulimalizika kwa Bayern kushinda mabao 2-0.

 

Julian: "Bayern Ilistahili Ushindi"

Bao zuri la kwanza kabisa kwa Leroy Sane liliwaweka mabingwa hao wa Ujerumani kwenye njia yao ya ushindi kabla ya Danilo D’Ambrosio kujifunga pale ambapo alitaka kuokoa shuti kali la Sane na kusababisha mchezo kuisha.

Julian Nagelsman aliwaambia waandishi wa habari kuwa, “Nimefurahishwa na matokeo ya mchezo wa leo.Tulikuwa na nguvu nzuri katika dakika zote 90. “Katika vipindi vyote viwili, tulikuwa na muda wa dakika 10 ambapo tulimpa nafasi mpinzani na wapinzani wetu wanaweza kucheza.”

Kocha huyo anasema kutokana na kuwa walistahili kushinda mechi hiyo, kupata alama tatu ndio ilikuwa kitu cha kwanza muhimu na anaamini kuna kitu kingine wanatakiwa kufanya pale wanapowinda mataji kama vile kuboresha maeneo mbalimbali.

 

Julian: "Bayern Ilistahili Ushindi"

Mechi inayofata ya michuano hii ya UEFA watakabiliana na Barcelona wakiwa nyumbani kwao Allianz Arena ambapo alipoulizwa juu ya kukutana na mshambuliaji wa zamani Lewandowski alisema anasubiri kwa hamu kwani mchezaji huyo ni hatari sana mbele ya lango.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa