Kocha wa klabu ya Bayern Munich Julian Nagelsmann haelewi jinsi klabu ya Barcelona inavyojiendesha licha ya kuwa kwenye ukata mkubwa lakini bado wamekuwa wakitunisha misuli kwenye soko la usajiri.

Klabu ya Barcelona imefanikiwa kumsajiri mshambuliaji wa klabu ya Bayern Robert Lewandowski, licha ya kuwa na matatizo ya kiuchumi lakini bado wameweza kufanikisha usajiri huo.

Nagelsmann
Julian Nagelsmann

Julian Nagelsmann amebaki na maswali mengi kichwani kwani alipokuwa akifanyiwa mahojiano na Tobi Altschäff alinukuliwa, “Barcelona, ni Klabu pekee ambayo haina hela lakini wananunua kila mchezaji wanayemtaka.

Sijui wanafanyaje. Ila ni ajabu, ina shangaza, ina pagawisha,” Nagelsmann alijibu wakati akiulizwa kuhusu usajiri.

Klabu ya Barcelona ina ukomo wa matumizi kwa sasa, kutokana na kanuni za kifedha zilizowekwa na La liga, ambazo zinaitaka klabu hiyo kutumia kiasi cha £1milioni kwa kila £4milioni ambayo wanaipunguza.

Awali ilitarajiwa kuwa klabu ya Barcelona kabla ya kufanikisha sajiri walizofanya, wangewapunguza wachezaji kama Frenkie de Jong na Ousmane Dembele, lakini ni tofauti na ilivyotarajiwa huku Dembele akijiandaa kusaini mkataba mpya na miamba hiyo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa