Mshambuliaji wa kimataifa kutoka nchini Argentina Amejiunga rasmi na klabu ya Roma kwa uhamisho huru na kusaini kandarasi ya miaka mitatu huku kukiwa na kipengere cha thamani ya €20milion kwa klabu itakayotaka kuvunja mkataba wake.

Paulo Dybala kabla ya kusaini Roma alihusishwa na vilabu vingi barani Ulaya vikiwemo vilabu vikubwa nchini Uingereza kama Tottenham na Arsenal, Lakini ameamua kubaki nchini Italia.

Roma, Roma wakamilisha Usajiri wa Paulo Dybala, Meridianbet

“Siku ambayo imenipelekea kusaini mkataba huu imejawa na hisia nyingi, uharaka na nia ambayo klabu ya Roma imetumia jinsi ilivyonihitaji mimi imeweka utofauti mkubwa.

“Najiunga kwenye timu ambayo iko kwenye kilele, klabu ambayo imeendelea kuweka misingi imara kwa ajiri mafanikio ya mbeleni, na kufanya kazi na jose mourinho itakuwa ni heshima.”

Dybala kwenye misimu yake saba aliyokuwepo kwenye klabu ya Juventus amefanikiwa kufunga magoli 115 kwenye michezo 293.

 

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa