Klabu ya Napoli inayoshiriki ligi kuu ya Italia Serie A imepinga taarifa zilizosambazwa na vyombo vya habari nchini humo kuwa klabu hiyo imeuzwa.

Vituo kadhaa vya runinga nchini humo vikiongozwa na kituo cha serikali Rai, vilieleza kuwa klabu hiyo imifikiana makubaliano ya kuuzwa kwa klabu hiyo kwa kiasi kinachokadiliwa kufikia €650 million.

Napoli, Napoli Yakana Kuuzwa kwa Klabu Hiyo, Meridianbet

 

“Kwenye hali yoyote ya kawaida, taarifa kama hii tusingehitaji kukataa lakini taarifa ya Rai kama chombo cha serikali wametulazimisha kusema hili. De Laurentiis hana nia ya kuiuza Napoli na hakuna mazungumzo yoyote.

“Awali, hapo nyuma, alikataa offer inayokaribia $1 billion. Kuibuka kwa tetesi ni kwa sababu raisi De Laurentiis kuwa angependa kuishi Marekani.

Napoli, Napoli Yakana Kuuzwa kwa Klabu Hiyo, Meridianbet

“De Laurentiis amekuwa akiishi jijini Los Angeles na Italia na hivi karibuni amerejea kwa miezi kadhaa kutoka kwenye makazi yake ya muda mrefu.

“Haitaji kuiuza Napoli kwa ajiri ya kuhamia Marekani pindi kazi zake zikimuhitaji.”

De Laurentiis, aliinunua klabu ya Napoli mwaka 2004 kipindi ambacho klabu hiyo ilikuwa miongoni mwa klabu tabu ambazo zilikuwa zinakwenda kufirisika.

De Laurentiis mara kwa mara amekuwa akipongezwa kwa utendaji na usimamizi mzuri wa klabu hiyo na kuwa klabu pekee kwenye serie A kutengezeneza faida mara kwa mara.

 

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa