Azam FC wamefunguka kwa kuweka wazi kuwa wanatamani kucheza mchezo wa kirafiki na klabu ya Simba nchini Misri ambako klabu hiyo imepanga kwenda kuweka kambi kwa ajiri ya kujiandaa na michezo ya ligi na mashindano yanayowakabili kwa msimu unaonza August.

Kikosi cha Azam FC kwa sasa kimeanza mazoezi ya awali kwenye Uwanja wao wa Azam Complex huku Julai 22, mwaka huu wakitarajia kwenda mji wa El Gouna, Misri kwa ajili ya kuweka kambi ya kujiandaa na msimu ujao.

Azam

Akizungumzia kambi yao, Kocha Mkuu wa Azam FC, Abdihamid Moallin amesema kuwa matamanio makubwa watakapoenda Misri ni kucheza na Simba kwani wanacheza ligi moja.

“Timu imeanza maandalizi kwa ajili ya kujiandaa na msimu ujao kabla ya kuelekea nchini Misri ambapo tutaweka kambi yetu na wachezaji wana morali ya kutosha.

“Tumeanza na programu ya asubuhi kuwa gym na jioni uwanjani ili kuwaweka fiti kwani walikuwa na likizo kidogo pia tunawaandaa kisaikolojia ili waweze kuwa sawa kuelekea msimu ujao.

“Tunatarajia kucheza mechi nyingi za kirafiki tukiwa pale Misri, tunafahamu kwamba na Simba nao wako kule kuna uwezekano wa kucheza hivyo tunatamani kucheza nao kwani na wao wanashiriki ligi ya Tanzania itakuwa mechi nzuri kwani itakuwa kipimo kizuri kwa wachezaji kujua zaidi ligi ilivyo.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa