Ofisa habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru ameteuliwa kuwa balozi wa mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ya Cambiasso.

Mashindano hayo yatajumuisha timu kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Montpellier HSC kutoka Ufaransa, Aigle Noir kutoka Burundi, KCCA kutoka Uganda pamoja na Janza Soccer School kutoka Zambia.

Kifaru

Huku kwa upande wa Tanzania zitashiriki timu nane ikiwemo Cambiasso Sports, Simba SC, Yanga SC, Ruvu Shooting, Zanzibar Combine, Azam FC pamoja na Mabingwa wa Ligi ya vijana Mtibwa Sugar.

Akizungumzia hilo Kifaru amesema kuwa: “Ni heshima kubwa kwangu kupewa nafasi hii ya ubalozi na Uongozi wa mashindano haya, naamini kuwa jitihada zangu ndizo zilizonifanikisha kufikia hatua hii ukizingatia kuwa timu ya vijana ya Mtibwa Sugar pia itashiriki mashindano haya.

“Timu kutoka nje ya nchi zimeshaanza kiwasili kwaajili ya mashindano haya ikiwemo timu ya Montpellier HSC ambayo tulienda kuipokea Jana majira ya saa nane mchana katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa