Thobias Kifaru, Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar ameweka wazi kuwa kwa sasa wanavuta pumzi kidogo wakijipanga kufanya kweli kwenye usajili mara baada ya kubaki kwenye ligi.

Mtibwa Sugar ilikuwa inapambana kubaki ndani ya ligi baada ya kumaliza ikiwa nafasi ya 13 na pointi 31 iliweza kufanikiwa kujihakikishia nafasi ya kubaki baada ya kushinda hatua ya mtoano mbele ya Tanzania Prisons kwa jumla ya mabao 3-2.

Kifaru

Kifaru aliweka wazi kuwa walikuwa na msimu mbovu lakini walifanikiwa kupambana na kubaki kwa ajili ya wakati ujao.

“Imani yetu ni kwamba mashabiki na sisi viongozi, wachezaji hatukupenda mwendo wetu mbovu kwa kuwa tumebaki tutafanya usajili mzuri na tutarejea kwa kasi kubwa msimu ujao,” alisema Kifaru.

Tanzania Prisons wao wanakibarua cha kusaka ushindi mbele ya JKT Tanzania kwenye mchezo wa mtoano, ambapo kwenye mchezo wa awali waliweza kushinda bao 1-0 ugenini, hivyo mechi ya mwisho itaamua nani atabaki kwenye ligi ama kushiriki Championship.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa