BAADA ya kuibuka na ushindi katika mchezo wa mtoano ‘playoff’ dhidi ya Tanzania Prisons, Uongozi wa Mtibwa Sugar umefunguka kuwa ilikuwa bahati mbaya wao kucheza hatua hiyo.

Mtibwa wamebaki katika ligi kuu baada ya kuibuka na ushindi wa jumla wa mabao 3-2 dhidi ya Prisons.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amefunguka kuwa

“Tumefurahi sana kubaki katika michuano ya ligi kuu kwa msimu ujao. Kazi tuliimaliza kwenye mchezo wa kwanza huu mchezo wa pili ulikuwa wa kukamilisha tu na hadi tunafikia huku tuliteleza hivyo kwa sasa tunaweka mikakati ya msimu ujao.”

Mtibwa Sugar wanasalia na kibarua cha kuboresha kikosi na kupambana vyema msimu ujao wa ligi ili kuendana na mchaka mchaka wa soka la msimu ujao.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa