UNAWEZA kusema kwamba Azam FC wana jambo lao kwa msimu ujao hiyo ni baada ya kutangaza kwamba wanatarajia kuweka kambi yao katika mji wa El Gouna uliopo nchini Misri.

Kikosi hicho kinatarajia kwenda huko kwa ajili ya kuweka kambi ya maandalizi ya msimu ujao ambapo timu itaanza kuweka kambi Dar es salaam kuanzia Julai 18.

Azam FC, Azam FC Wana Jambo Lao, Meridianbet

Akizungumzia kambi hiyo, Ofisa Habari wa Azam Fc, Thabit Zakaria ‘Zaka zakazi’ alisema kuwa “Azam inatangaza kwamba itaenda Misri kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya katika mji wa El Gouna uliopo Misri.

“Ni mji wa kitalii, ni eneo zuri sana kwa ajili ya kujitenga kwa maandalizi, kutokana na utulivu na miundo mbinu mizuri, timu itaondoka Julai 22 na itakuwa huko hadi Agosti 12 na itarudi Dar.

“Kabla ya kuondoka wachezaji wote watakuwa wamewasili kwa ajili ya kambi itakayoanza Julai 18 hivyo wachezaji wataanza kuwasili kuanzia Julai 15 hadi 17 kwa ajili ya mchakato mwingine ikiwemo vipimo.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa