KIPA namba moja wa Simba, Aishi Manula ameweka wazi viongozi wa timu yake wamekuwa mstari wa mbele kubariki kuweza kupata changamoto mpya ikiwa atapata sehemu nzuri.
Manula mwenye clean sheet 11, amefungwa mabao 11 kwenye mechi 21 alizocheza, huku akitumia dk 1,890. Manula anatajwa kuongeza dili la miaka miwili ndani ya timu hiyo, ambayo imepoteza mataji yake matatu iliyotwaa msimu wa 2020/21, ila imeweza kutapoteza yote msimu wa 2021/22.

Simba, Simba Wabariki Manula Kuondoka, Meridianbet

Kipa huyo amesema: “Sidhani kama Simba wamesema nimeongeza mkataba, meneja wangu alichapisha kwenye mitandao ya kijamii tukiwa kwenye mazungumzo, sidhani kama meneja wangu wangu Jemedari Said alisema kwamba deal done.

“Nadhani Watanzania wanahitaji kuona napata mafanikio na Simba, wamesema kuwa kama nitapata sehemu ya kwenda wapo tayari kuniachia niweze kwenda, ikiwa nitapata sehemu bora zaidi, wao wamesema hawana tatizo.

“Klabu yangu ya Simba mara zote wamekuwa wakisema hawana tatizo. Viongozi wangu wamekuwa na mawazo chanya, ikiwa ninaweza kupata sehemu wao watakuwa mstari wa mbele kuhakikisha naondoka na naendelea kupata mafanikio nje ya Simba.

“Msimu ulikuwa mzuri kwa bahati mbaya klabu ilikuwa ni msimu mbaya kwetu, kwa sababu sio vile ambavyo tulikuwa tumezoea hasa kwa kushindwa kupata mataji tuliyokuwa tunahitaji,” amesema.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa