Kocha mkuu wa klabu ya Atletico Madris Diego Simeone amesema kuwa mchezaji Antoine Griezman ni mchezaji muhimu sana katika historia ya Atletico Madrid kutokana na uwezo wake alionao.

 

Simeone: Griezmann ni Muhimu Sana

Simeone amesema hayo kutokana na Antoine kufunga bao la pili katika mchezo wa jana wa michuano ya klabu bingwa dhidi ya FC Porto ambao ulimalizika kwa Atletico kushinda kwa mabao 2-1. Mechi hiyo ilikuwa na ugumu wake kwani timu hizi zilipata mabao katika dakika za nyongeza. Aliongezea kwa kusema kuwa,

 

Simeone: Griezmann ni Muhimu Sana

“Nampenda sana mchezaji huyu” alisema katika mkutano na waandishi wa habari, “Mbali na mapenzi kwake, ni mmoja wa wachezaji muhimu katika historia ya klabu. “Tutaendelea kuimarika. Anatupa mengi na lazima awe na nguvu kichwani.

Vijana wa Simeone ndio walianza kupata bao dakika ya 91 baada ya Porto kupata kadi nyekundu dakika ya 81 na baadae kwenye dakika ya 96 Porto kuchezewa madhambi walipata bao la kusawazisha kwa mkwaju wa penalty, lakini haishuia hapo dakika ya 101, Griezman alitupia kambani bao la pili  kwa upande wao na kufanya wainuke wababe kwenye mchezo huo ambao walikuwa ndio wenyeji wa mchezo huo.

Atletico Madrid baada ya ushindi huo, mchezo unaofuata kwenye michuano hii watamenyana na Bayer Leverkusen ugenini. Leverkusen ambao wametoka kupoteza mchezo wao wa kwanza dhidi ya Club Brugge kwa bao 1-0.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa