UONGOZI wa Simba jana mchana ulitangaza kuvunja mkataba na kocha wake Mserbia Zoran Manoljović (60) baada ya kudumu kwa miezi miwili huku sababu tatu zikitajwa kumuondoa.

Huyo ni kocha wa pili wa kigeni kutimuliwa tangu kuanza kwa msimu huu, mwingine ni kaimu Kaimu Kocha Mkuu wa Azam FC, Abdihamid Moallin raia wa Somalia na Marekani.

Zoran, Hizi Hapa Sababu za Zoran Kutimuliwa Simba, Meridianbet

Simba ilimuajiri na kumtangaza kwa mbwembwe Zoran Juni 28, mwaka huu akichukua nafasi ya Mfaransa, Franco Pablo.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa mmoja wa mabosi wa timu hiyo, sababu tatu za msingi ambazo zimemuondoa kocha huyo kuendelea kukinoa kikosi hicho huku mshambuliaji wa timu hiyo, Mserbia Dejan Geogjivic akipewa muda wa kuangaliwa.

Bosi huyo alizitaja sababu hizo ya kwanza ni Kuishiwa mbinu kwa kocha kwa siku zote alizokaa na timu hiyo akiifundisha ameonekana kuishiwa mbinu za kuipa matokeo mazuri ya ushindi katika michezo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa