Simba sports club mabingwa wa zamani ligi kuu nchini Tanzania wamemalizana na kocha wao aliehudumu kwa muda mfupi klabuni hapo Mserbia Zoran Maki.
Klabu ya Simba imetoa taarifa ya kuachana na kocha huyo muda mfupi uliopita na wakieleza wamefikia makubaliano ya pande zote mbili na kocha huyo aliejiunga na klabu hiyo mwishoni mwa mwezi wa sita akiwa amedumu klabuni hapo kwa takribani miezi miwili na siku kadhaa.
Zoran amefanikiwa kuiomgoza timu hiyo kwenye mechi tofauti kuanzia zile za kujiandaa na msimu kule nchini Misri,Simba day pia mechi za ushindani kocha huyo anaondoka akiwa amefunga kwenye ngao ya jamii dhidi ya watani zao Yanga pia akiwa ameshinda mechi mbili za awali za ligi kuu na kuongoza ligi mpaka sasa.
Habari zinaeleza kocha huyo amepata ofa kubwa kutoka klabu moja nchini Misri ndio sababu ya yeye kuhitaji kuondoka kwenye viunga vya msimbazi pia klabu ya simba imeeleza kuachana na kocha viungo Sbai Karim pamoja na Rachid Mohamed.
Kwa wakati huu klabu ikiwa ianatafuta kocha mpya Simba wameeleza aliekua kocha msaidizi Selemani Matola atakaimu nafasi hiyo mpaka kocha mpya atakapopatikana taarifa ya Simba ilieleza hivo.

