Ten Hag kocha wa klabu ya Manchester United ameeleza kua hatma ya mshambuliaji wake raia wa Uingereza Marcus Rahford ipo mikononi mwa klabu hiyo.

Ten hag ambaye anaoneshwa kufurahishwa na kiwango cha nyota huyo toka kuanza kwa kwa msimu huu amesema anachoamini klabu hiyo itapambana kumuongezea mkataba mchezaji huyo baada ya kua na tetesi siku kadhaa kua nyota huyo anaweza kutimkia kwenye klabu ya PSG miamba ya soka nchini Ufaransa.

ten hagMkataba wa Rashford unamalizika mwishoni mwa msimu huu lakini kocha huyo naamini mustakabali wa mchezaji huyo upo mikononi mwa klabu kwakua kijana huyo yupo kwenye mipango ya muda mrefu ya timu hiyo.

Rashford ambae alifunga mabao matano tu msimu ulioisha kwenye michezo yote lakini akionekana kua na kiwango kizuri msimu huu kwani ana mabao matatu na pasi mbili za mabao mpaka sasa hivo kuonesha anaweza kurejesha makali yake ndani ya klabu hiyo.

Kocha huyo ameongeza anachokiana kwa Rashford ni mwenye furaha na anataka kupambana kitu ambacho kitakua msaada kwa timu.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa