Beki wa kati  wa timu ya Taifa ya Ufaransa na Manchester United Raphael Varane amemsifia “sifa kedekede” Ousmane Dembele na anaamini kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 hatimaye “anachanua” ndani ya Barcelona.

 

Varane Aukubali Uwezo wa Dembele

Dembele amekuwa mchezaji aliyezaliwa upya tangu Xhavi alipoanza kuinoa klabu hiyo Novemba 2021 huku pasi zake 17 za mbao katika michuano yake yote zikizidiwa na Lionel Messi (22), De Bruyne (21) na miongoni mwa wachezaji wa ligi tano bora za Ulaya, huku assist zake 15 za Laliga wakati huo anawakilisha ligi ya juu.

Mchezaji huyo wa zamani wa Borrusia Dortmund pia anaongoza chati za Barca kwa kutengeneza nafasi 63, nafasi zilizotengenezwa kutokana na mchezo wa wazi (52) na klugusa kwenye sanduku la mpinzani (126) chini ya Xhavi kwenye Laliga.

Dembele alisaini mkataba wa miaka miwili na Barca mwezi Julai, na Varane anafikiri kuwa na ubora wa ajabu . Alisema kuwa;

 

Varane Aukubali Uwezo wa Dembele

“Nimefurahi sana kumuona katika kiwango hiki” alisema tunamwona akichanua. Ana sifa za ajabu. Pia ni mtulivu zaidi, daima kimya. Ameweza kupata kichocheo cha kupona kimwili, kujisikia vizuri, na tuna furaha sana” .

Varane alisema kuwa Dembele alikuwa na majeraha ambayo yalifuatana, lakini sasa tunayo nafasi ya kumuona akiburudika na kufurahia uwanjani, kwahivyo sote tuna furaha kubwa”. Hakuishia hapo beki huyo aliusifu uwezo wa mchezaji mwenzake wa Kifaransa Aurelien Tchouamen katika klabu yake ya zamani ya Real Madrid .

Tchouamen ambaye alijiunga na Real kutoka Monaco mwezi Juni ameanza vizuri msimu kwa kiwango cha kuvutia kwenye kikosi cha Ancelotti, na Varane anaamini kwamba ana ukomavu wa kuendelea kuwa bora zaidi.

 

Varane Aukubali Uwezo wa Dembele

“Hasiti katika uteuzi wake wa kwanza wa kuomba mpira, kuvuta pumzi, na kwa umri wake mdogo tayari amekomaa sana na ninatamani abaki kwenye mkondo, aendelee hivi, kwa anachofanya tayari ni cha ajabu”.

 

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa