Wachezaji wawili wa Manchester United Raphael Varane na Paul Pogba wote wanatarajiwa kuwepo kwa mechi ya Jumamosi ya Ligi Kuu dhidi ya Leicester City kwenye Uwanja wa Old Trafford.
Awali kuliibuka wasi wasi juu ya uwepo wa wachezaji hao wawili wa Ufaransa kwenye mechi hiyo baada ya kuwa na majeraha walipokuwa wakiwakilisha nchi yao.
Varane alilazimika kutoka nje katika ushindi wa timu yake ya taifa dhidi ya Ivory Coast siku ya Ijumaa kutokana na tatizo la mguu, wakati Pogba hakuweza kumaliza mazoezi ya Jumapili baada ya kukumbana na tatizo kama hilo.
Hata hivyo, Varane alicheza dakika 80 za ushindi wa Ufaransa wa mabao 5-0 dhidi ya Afrika Kusini Jumanne, baada ya kutangazwa kuwa anafaa kuingia uwanjani.
Pogba alitoka kwenye kikosi cha kwanza kwenye mechi ya kirafiki lakini aliwekwa benchi na kucheza dakika 25 za mwisho, akichukua nafasi ya Olivier Giroud.
Kutokana na hali hiyo, wachezaji wote wawili wanatarajiwa kuwepo na Man United wikendi hii, huku kikosi cha Ralf Rangnick kikitarajia kurejea katika njia ya ushindi kufuatia kukatishwa tamaa kwenye Ligi ya Mabingwa.
3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!
Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.