Man United Wana Mpango wa Kumtumia Martial kwa Kane!

Manchester United wanaripotiwa kutarajia kumjumuisha Anthony Martial katika uhamisho wa mshambuliaji wa kati wa Tottenham Hotspur Harry Kane msimu wa joto.

TMashetani wekundu watasajili mshambuliaji mpya wakati dirisha la usajili la majira ya joto na inadaiwa wanafikiria kutoa ofa ya pesa nyingi kwa Kane, ambaye alishindwa  kuhamia Manchester City msimu uliopita wa joto.

Man United Wana Mpango wa Kumtumia Martial kwa Kane!
Harry Kane

Spurs bado wanamthamini nahodha huyo wa England kwa zaidi ya £100m licha ya kwamba mkataba wake umebakiza miaka miwili tu kumalizika, lakini kwa mujibu wa ESPN, Man United wanafikiria kumhusisha Martial kama sehemu ya dili la kubadilishana.

Ripoti hiyo inadai kuwa Tottenham wanamkubali Martial kwa muda mrefu, ambaye atatumia muda wote uliosalia kwa mkopo huko Sevilla kabla ya kurejea Old Trafford.

Martial amefunga mara moja na kutoa asisti moja katika mechi nane alizoichezea Sevilla, ambao hawana uwezekano wa kumsajili kwa mkataba wa kudumu mwishoni mwa kampeni.


3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!

Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.

Kubeti Poa - Bonasi Kubwa

Jisajili sasa

Acha ujumbe