Maguire Azomewa Wembley Stadium.

Maisha ya wachezaji ni changamoto kwa sehemu kubwa. Harry Maguire ni mfano halisi wa ugumu wa maisha yao ndani na nje ya uwanja.

Nchini Uingereza, dau unalosajiliwa nalo, linapaswa kuendana na uwezo, mchango na matokeo yako uwanjani. Haya ndiyo mategemeo ya mashabiki wa vilabu vya uingereza. Kukisekana uwiano wa pesa iliyotolewa na mchango wa mchezaji husika, hasira za mashabiki huwa ni kali siku zote.

Harry Maguire amekutana na joto ya jiwe akiwa kwenye uwanja wa nyumbani. Huyu ni nahodha wa Manchester United na muhimili imara kwenye kikosi cha Timu ya Taifa ya Uingereza. Ukitizama vizuri, kuna uwiano wa Paul Pogba na Harry wanapokua kwenye timu za taifa.

Maguire

Kwenye ngazi ya klabu, wachezaji wote wawili hawachezi kwenye kiwango kinachotarajiwa kutoka kwao lakini, wakiwa na timu zao za taifa wanafanya makubwa na kupambana kwa kila hali. Kwanini hawafanyi hivyo wakiwa Man United?

Mashabiki wameamua kumtolea uvivu Maguire kwenye mchezo dhidi ya Ivory Coast kule Wembley Stadium. Licha ya kuwa mchezaji mhimu kwenye timu ya Uingereza, alijikuta akizomewa na sehemu kubwa ya mashabiki waliohudhuria mchezo huo. Kuzomewa kwa Harry kumezua hali ya kufikirisha kwa kocha wa timu hiyo, Gareth Southgate na baadhi ya wachezaji wenzake.

Inaaminika kuwa, kuzomewa kwa Harry hakutokani na uwezo wake akiwa na timu ya taifa bali ni kiwango duni anachokionesha United licha ya kusajiliwa kwa pesa ndefu kwenye historia ya EPL (kwa mabeki).


3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!

Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.

Kubeti Poa - Bonasi Kubwa

Jisajili sasa

Acha ujumbe