Klabu ya Atlético Madrid imeripotiwa kuwa tayari kumuuza mshambuliaji wake wa kimataifa wa Argentina Julián Álvarez katika dirisha lijalo la usajili wa majira ya kiangazi kwa timu yoyote ya Premier League itakayokuwa tayari kulipa ada ya pauni milioni 85.
Hata hivyo, viongozi wa Atletico wamesisitiza kuwa hawapo tayari kupokea ofa yoyote kutoka kwa wapinzani wao wa ndani, FC Barcelona, licha ya uwezekano wa klabu hiyo kuonyesha nia ya kumsajili nyota huyo.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Uamuzi huo unatokana na ushindani mkubwa uliopo kati ya klabu hizo mbili ndani ya soka la Hispania, hali inayofanya Atletico kutotaka kumuimarisha mpinzani wao wa moja kwa moja.
Wakati huo huo, klabu ya Arsenal FC imekuwa ikitajwa mara kadhaa kuonyesha nia ya kumsajili Alvarez, ingawa ada kubwa ya uhamisho imeonekana kuwa changamoto kwa timu hiyo ya London.
Inaelezwa kuwa Arsenal wanaamini kuwa mshambuliaji huyo anaweza kuongeza makali katika safu yao ya ushambuliaji, ambayo licha ya kufanya vizuri msimu huu bado inaonekana kuhitaji maboresho zaidi.
Kwa upande wake, Alvarez anaripotiwa kuwa na hamu ya kurejea tena katika Ligi Kuu England kutokana na uzoefu wake wa awali katika ligi hiyo.

