Armando Broja ametia saini mkataba mpya wa miaka sita na Chelsea utakaomfanya atumikie klabuni hapo hadi 2028. Broja anacheza katika eneo la ushambuliaji, ambalo ndilo ambalo limekuwa likiisumbua Chelsea kwa muda sasa.

Kocha wa timu hiyo Thomas Tuchel alimtaka Broja asalie klabuni hapo baada ya kuwa na mapendekezo mengi ya kumtaka mshambuliaji huyo Muingereza. Armando anasema kuwa amekosa maneno ya kuongea kwani timu hiyo ilikuwa ni klabu yake ya ndoto kuichezea toka alipokuwa mtoto. Aliendelea kusema kuwa,
“Chelsea ni klabu ninayoishabikia, na klabu ninayoipenda. Nimekuwa hapa toka nilipokuwa mvulana, hivyo ni hisia ya ajabu kwangu na familia yangu”.

Armando anaenda kuungana na kina Sterling, Harvetz, Ziyech, Aubameyang, na wengine wengi katika eneo la ushambuliaji na huenda wakafanikisha kupata mabao mengi kupita msimu ulipita.
Imekuwa ni jambo zuri kwa Chelsea kumbakiza mchezaji huyo kwani Tuchel atakuwa na faida kuelekea michuano ya klabu bingwa Ulaya ambayo inatarajiwa kuanza siku ya Jumanne ambapo Chelsea atakuwa ugenini akicheza dhidi ya Dinamo Zagreb.

