Antony Matheus dos Santos winga wa kibrazil aliesajiliwa kwa gharama zaidi kunako ligi kuu ya uholanzi inaelezwa ataelezwa jezi namba 21 mdani ya Manchester United.
Winga huyo hatari aliesajiliwa kutoka klabu ya Ajax ya nchini Uholanzi na kuweka rekodi ya ya dau kubwa la usajili kwenye ligi hiyo ametua klabuni Manchester United na kuungana na mwalimu wake wa zamani wa klabu hiyo Eric Ten hag.
Nyota huyo inaelezwa atavaa jezi namba 21 tofauti na ilivyoelezwa mwanzo kua atavaa jezi namba 11 iliokua ikivaliwa na kinda wa klabu huyo Mason Greenwood ambae bado yupo nje ya uwanja kutokana na kesi inayomkabili kutokana na hali hiyo ni wazi kua kinda huyo ana uwezekano wa kurejea klabuni hapo.
Mchezaji huyo alietambulishwa klabuni hapo siku ya alhamisi mchana ameahidi kuipambania klabu kwa uwezo wake wote na kurudisha klabu sehemu inayostahili kuwepo.

