Marcelo( 34)Kujiunga Olympiacos

Gwiji wa Real Madrid Marcelo yupo tayari kujiunga na Olympiacos ya nchini Ugiriki kwa uhamisho huru. Marcelo ambaye ni mchezaji wa timu ya Taifa ya Brazil anacheza katika nafasi ya beki wa kushoto.

Marcelo( 34)Kujiunga Olympiacos

Marcelo amedumu katika klabu ya Real Madrid ya Hispania kwa muda mrefu ambapo alijiunga na mabingwa hao mara nyingi wa michuano ya klabu bingwa barani Ulaya mwaka 2015 na kupata nayo mafanikio mengi yakiwemo makombe ya ligi, makombe ya Uefa, makombe ya Copa Del Rey, na mengine mengi.

Baada ya ujio wa Carlo Ancelotti imekuwa ni vigumu kwa beki huyo kupata namba ya mara kwa mara kwa mabingwa watetezi wa Laliga msimu uliopita, Hivyo akaona ni bora atafuta changamoto kwingine kwani ameshapata mafanikio na klabu hiyo.

Marcelo( 34)Kujiunga Olympiacos

Marcelo anaenda kujiunga na Olympiacos kwa mkataba utakaomuweka klabuni hapo hadi Juni 2023 na chaguo la kurefusha mkataba likiwemo hapo baadae. Beki huyo anatumaini kupata nafasi ya kucheza mara kwa mara katika klabu yake mpya kwasababu ya uzoefu wake.

Acha ujumbe