Nahodha msaidizi wa Klabu ya Yanga SC, Dickson Job, amefanyiwa upasuaji wa goti baada ya kuumia vibaya katika mchezo wa Dabi ya Kariakoo dhidi ya Simba SC uliofanyika Machi 1 kwenye Uwanja wa Amani Complex visiwani Zanzibar.

Jeraha hilo lilitokea baada ya kugongana na kiungo mshambuliaji wa Simba, Inn Loemba, jambo lililosababisha hitaji la upasuaji wa haraka ili kurekebisha goti lake. Upasuaji huo umefanyika nchini South Africa na kwa muujibu wa ripoti za madaktari wanasema kwamba Job atahitaji muda wa miezi kadhaa kupumzika na kupona kikamilifu kabla ya kurejea kwenye kikosi cha kwanza cha Yanga.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Kukosa Job uwanjani kunakuwa pigo kwa Yanga SC kwani yeye ndiye mmoja wa wachezaji muhimu katika safu ya ulinzi na kuongoza timu, na klabu itahitaji kupanga mbinu mbadala ili kudumisha ushindani katika Ligi Kuu Bara na michuano ya kombe la shirikisho la CRDB.

