Ripoti kutoka Italia zinadai kuwa Juventus wanapanga kurejea tena katika wazo la kumsajili Granit Xhaka kwenye dirisha la usajili la Januari, zikiwa ni miezi sita tu tangu arejee Ligi Kuu ya England akichezea Sunderland.

Kwa mujibu wa jarida la Italia Tuttosport, Juventus wanataka kuongeza nguvu kwenye eneo lao la kiungo, ambalo kwa sasa linategemea mno huduma za Khephren Thuram na Manuel Locatelli, na kwa sababu hiyo, wanafikiria tena kumchukua Xhaka.
Kiungo huyo wa kimataifa wa Uswizi alikuwa miongoni mwa chaguo la Juventus wakati wa dirisha la majira ya kiangazi, kipindi ambacho alikuwa anapatikana kwa ada ya takriban €15m. Hata hivyo, taarifa za Jumanne zinaeleza kwamba Xhaka hakutimiza vigezo vyote vya Juventus wakati huo, hasa kutokana na umri wake, kwani alitimiza miaka 33 mwezi Septemba.
Leo hii unaweza kutusua mkwanja mrefu endapo utacheza michezo ya Kasino ya Mtandaoni kama vile Aviator, Poker, Roullette, Keno, Super Heli na mingine kibao. Ingia Meridianbet sasa na ucheze hapa.



