Mchezaji wa FC Barcelona Jules Kounde amesema kuwa alijiunga na timu hiyo badala ya kujiunga na Chelsea ambayo kwa wakati huo bado ilikuwa chini ya kocha mkuu Thomas Tuchel kwasababu  alipenda risala aliyopewa na kocha wa klabu hiyo Xhavi Hernandez.

 

Kounde Afichua Siri ya Kujiunga Barcelona

Mchezaji huyo wa Kimataifa wa Ufaransa alionekana kuwa tayari kusaini Chelsea wakati wa dirisha kubwa la usajili la hivi majuzi, lakini akaweka bayana kuhusu mkataba wa miaka mitano Camp Nou.

Mkurugenzi wa soka wa Sevilla Monchi alipendekeza kwa wakati huo ambapo  Barca walimnyakua Kounde baada ya Chelsea kuondoa ofa yao kutokana na “kuwa na mashaka” .Hata hivyo katika mahojiano na jarida la L’Equipe la Ufaransa  Kounde alisisitiza kuwa uamuzi huo ni wake mwenyewe baada ya kubembelezwa na kocha mkuu wa Barca Xhavi.

“Kwanza nimekuja kwenye klabu kubwa, ambayo imejua nyakati nzuri na ambayo hivi majuzi imeanza vizuri, Nilikuwa na nia ya kuwa sehemu ya wimbi hili jipya, kusaka mataji, na kuirejesha Barca pale ambapo imekuwa miongoni mwa vilabu bora zaidi.

 

Kounde Afichua Siri ya Kujiunga Barcelona

Aliendelea kusema kuwa aliongea pia na Tuchel lakini aliipenda hotuba ya Xhavi zaidi. Chelsea walianza taratibu sana msimu huu ambapo ulifanya wamtimue Tuchel. Wakati kwa upande wa Barca wao walianza vizuri msimu licha ya kuwa na hali ngumu ya kifedha  ambapo mpaka sasa wapo nyuma nafasi mbili dhidi ya vinara Real Madrid.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa