Real Madrid Kukipiga na Man United Usiku wa Leo

Klabu ya Real Madrid inatarajia kushuka dimbani usiku wa leo kukipiga na klabu ya Manchester United nchini Marekani katika mchezo wa kujiandaa na msimu ujao.

Mchezo kati ya Real Madrid na Man United ni moja ya michezo yenye mvuto zaidi duniani kwani ni timu ambazo zina mashabiki wengi zaidi ulimwenguni hivo wanapokutana mara nyingi mchezo unakua wenye mvuto mkubwa.Real MadridMchezo huo unatarajiwa kupigwa katika jiji la Houston usiku wa leo ambapo vikosi vya timu zote tayari vimeshafika katika jiji hilo wakisubiria mtanange huo ambao unasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka nchini humu na duniani kwa ujumla.

Timu hizo zimeshawahi kukutana nchini Marekani katika mchezo wa kujiandaa na msimu mpya kama huu mwaka 2014 na uliishia kuweka rekodi kubwa ya kujaza mashabiki kwani mchezo huo uliingiza mashabiki 109,318.Real MadridVilabu vya Real Madrid na Man United ambavyo mara ya mwisho vilipokutana nchini Marekani viliweka rekodi ya kujaza mashabiki wengi katika mchezo huo, Lakini pia mwaka huu wamefanikiwa kumaliza tiketi mwanzoni mwa mwezi huu ambapo tiketi za mchezo zilikua zimeshamalizika.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.