Cristiano Ronaldo aliliambia kundi la mashabiki wa Manchester United wenye shauku watulie walipokuwa wakitafuta picha yake baada ya mechi kwenye Uwanja wa Old Trafford, akilinganisha na ule mtindo wake wa ushangiliaji wa yake ‘Calma’.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37 amekuwa na msimu mgumu akiwa na United, ndani na nje ya uwanja baada ya kuiambia klabu kuwa anataka kuondoka msimu wa joto na kukataa kutoka benchi katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Tottenham Hotspur.

Lakini hilo halijamzuia mshindi huyo mara tano wa Ballon d’Or kuabudiwa na mashabiki wa Red Devils. Hata wewe ni mshindi wa leo kutoka meridianbet, tazama odds bomba hapa.
Na katika video mpya, supastaa huyo wa Ureno aliweza kuonekana akiwaonyesha mashabiki kwa ishara watulie huku wakipiga kelele na kupiga mayowe kutaka kusainiwa jezi na gwiji huyo wa United.

Katika video hiyo, Ronaldo anaonekana akisaini jezi ya shabiki huku wafuasi waliomzunguka wakiendelea kulitaja jina lake na kushikilia kalamu na kumbukumbu.
Fowadi huyo anatazama umati wa watu kabla ya kuinua mikono yote miwili juu, tofauti kidogo na mtindo wake ule wa kushangilia kwenye El Clasico dhidi ya Barcelona kwenye Uwanja wa Camp Nou, na kuwapa mashabiki ishara ‘Calma’ kwamba watulie.

