Baada ya mshambuliaji wa klabu ya Simba Dejan Georgijevic kuvunja mkataba na klabu yake, ambapo taarifa hiyo haikutoa rasmi katika klabu yenyewe bali alichapisha taarifa hiyo kwenye mtandao wa kijamii ambao ni Instagram na kuthibitisha hilo timu hiyo ikaamua kutoa neno pia.
Dejan alisajiliwa na Simba msimu huu katika dirisha kubwa la usajili hajafikisha hata miezi mitano klabuni, na pia hajaweza kuanza katika mechi takribani zote walizocheza wekundu wa msimbazi hadi.
Wakati mshambuliaji huyo anatua kwa Wanalunyasi klabu hiyo ilikuwa chini ya kocha mkuu Zoran Maki ambae nae alitimkia Misri kuinoa timu ya AL Ittihad baada ya kupata ofa nzuri ambayo alikuwa nalipwa zaidi ya aliyokuwa akilipwa Msimbazi.
Mshambuliaji huyo kutoka nchini Serbia mwenye umri wa miaka 28 amefunga bao moja tuu katika mechi alizocheza za NBC Primia ligi ambapo mechi hiyo ilikuwa ni dhidi ya Kagera Sugar ambapo mechi ilimalizika kwa Msimbazi kushinda kwa mabao 2-0 katika uwanja wa Benjamin MKapa.
Kutokana na mshambuliaji huyo kuvunja mkataba na klabu hiyo nayo imetoa taarifa kwa Umma kupitia akaunti yao ya Instagram, kuhusu kuvunja mkataba na mchezaji huyo wa Kiserbia ambapo kupitia akaunti yao ya Insta wamesema kuwa, wamesikitishwa na kitendo hicho cha mchezaji kuvunja mkataba kupitia mtandaoni na watachukua hatua stahiki kwa mchezaji huyo kuvunja mkataba bila kufuata taratibu maalumu.