Mkufunzi wa Atletico Madrid Diego Simeone amesema kuwa mzozo uliopo kati yao na wapinzani wao Real Madrid ni “Filamu Mpya” huku akisisitiza kuwa hali hiyo haina maana yoyote kuelekea mchezo wao wa Derby unaotarajiwa kwa hamu hapo Jumapili.

 

Simeone: "Tutakutana na Timu Kubwa Yenye Wachezaji Wazuri"

 

Miamba hao wawili wa Laliga wanajivunia bahati tofauti huku wakijiandaa kumenyana na Wanda Metropolitano  Jumatano. Los Rojiblancos wanalenga kurejea kutoka kwa kushindwa kwao Ligi ya Mabingwa katikati ya Juma dhidi ya Bayer Leverkusen, wakati Los Blancos ya Carlo Ancelloti wakiwa wameshinda kila mechi kati ya 8 katika michunano yote msimu huu.

Kocha wa Atletico Madrid Simeone alithibitisha kuwa mlinda mlango wake Oblak atakuwa fiti kuanza baada ya kupata ahueni baada ya kupata jeraha siku chache zilizopita ambapo amesema kuwa mchezo wa kwanza kati yao utawakilisha mwanzo mpya kwa timu hizo mbili.

Simeone: "Tutakutana na Timu Kubwa Yenye Wachezaji Wazuri"

 

Simeone alisema kwamba; “Siku zote huwa nafikiri kwamba katika michezo mikubwa na kwenye Derby, ni muhimu jinsi unavyofika,” Aliwaambia waandishi wa habari katika mkutano na waandishi wa habari  Jumamosi. ” Ningependa kuja na ushindi na kuangalia kila mara kutoka upande chanya”

Aliendelea kusema kuwa kila mchezo unapoanza ni hadithi mpya. Kila kitu ni kizuri sana hadi mwamuzi aanze; ni filamu mpya ambayo hatujui mwisho wake, ndiyo maana mchezo huu unafurahisha sana.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa