Klabu ya Tottenham Hotspurs imefikia makubaliano binafsi na mchezaji huyo wa klabu hiyo ya Leicester City James Maddison na mpaka kufikia hatua hiyo wako mbioni kumsajili mchezaji huyo.

Kiungo James Maddison amekua akifanya vizuri ndani ya klabu ya Leicester City na klabu hiyo kwasasa imeshuka daraja, Hivo kwake imekua fursa kutafuta klabu nyingine na Tottenham ndio wamekua chaguo lake la kwanza.TottenhamKiungo huyo wa kimataifa wa Uingereza amekua akifatiliwa na vilabu kadhaa ndani ya ligi kuu ya Uingereza kama Newcastle, Man United pia lakini vijogoo hao wa London ndio wanaonekana kukaribia kuinasa saini ya kiungo huyo.

Klabu ya Tottenham wanaonekana kufanya usajili kwa umakini mkubwa ili kuhakikisha wanarejea kwenye ubora wao msimu ujao, Kwani msimu uliomalizika wamekua na msimu mbovu sana hivo hawataki kurudia makosa tena.TottenhamMwenyekiti wa klabu ya Tottenham Daniel Levy inaarifiwa anataka kufanya kila kitu mapema ili kuhakikisha wanampata mchezaji huyo ili kukiboresha kikosi chao kuelekea msimu ujao na mpaka sasa kuna kila dalili mchezaji huyo atsaini kwenye klabu hiyo.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa