PSG Wachukua Beki Bayern Munich

Klabu ya PSG iko mwishoni kukamilisha usajili wa beki wa kimataifa wa Ufaransa anayekipiga klabu ya Fc Bayern Munich Lucas Hernandez kwajili ya kujiandaa na msimu ujao.

Klabu ya PSG imeshakubaliana na mchezaji Lucas Hernandez maslahi binafsi ambaye aliitaarifu klabu yake ya Bayern Munich anataka kuondoka ndani ya timu hiyo huku mabingwa hao wa Ufaransa wakiwa chaguo la beki huyo.PSGTaarifa zinaeleza kua uongozi mpya wa klabu ya Bayern Munich umempa masharti beki Lucas Hernandez na kumueleza achague kati ya kuongeza mkataba wa kubakia klabuni hapo au aondoke ndani ya timu hiyo na beki huyo amechagua kuondoka.

PSG msimu huu wameonekana kufanya sajili ambazo zinaonekana ni kwajili ya mradi wa muda mrefu klabuni hapo, Kwani sajili zao hazijalenga katika majina makubwa zaidi wanaonekana wanataka kusajili kwa mikakati zaidi.PSGLucas Hernandez amekua na misimu bora kadhaa ndani ya klabu ya Bayern Munich akitokea Atletico Madrid ya nchini Hispania, Lakini amefakia hatua ya kutaka kuondoka ndani ya timu hiyo na chaguo lake la kwanza limekua klabu ya PSG mabingwa soka nchini Ufaransa.

Acha ujumbe