Klabu ya Yanga SC imeweka wazi dhamira yake ya kutafuta ushindi katika mchezo wa hatua ya 16 bora ya Kombe la Shirikisho la CRDB, huku benchi la ufundi na wachezaji wakisisitiza umuhimu wa tahadhari dhidi ya wapinzani wao TMA.
Kocha Mkuu wa Yanga, Pedro Goncalves, amesema timu yake haiendi uwanjani kutafuta sare bali ushindi, akionya kuwa michezo ya mtoano huwa na changamoto kubwa hasa dhidi ya timu za madaraja ya chini. “Kesho hatuendi kutafuta alama bali ushindi. Timu za madaraja ya chini hucheza kwa nidhamu kubwa sawa na zile za ligi kuu, hivyo ni lazima tuwe makini na waangalifu,” amesema.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Ameongeza kuwa presha ipo kwa upande wa Yanga kwani kupoteza kunaweza kugharimu ndoto zao za ubingwa. “Tusipokuwa waangalifu tutajikuta kwenye hali ngumu kwa sababu wapinzani hawana cha kupoteza. Sisi tukipoteza tutakuwa tumepoteza ubingwa, lakini tukitekeleza kila jambo ipasavyo tuna nafasi nzuri ya kutwaa tena,” ameongeza Pedro Goncalves.
Kwa upande wake, kiungo mshambuliaji Allan Okello amesema wachezaji wana morali kubwa na wako tayari kupambana ili kupata ushindi ndani ya dakika 90, huku akisisitiza umuhimu wa nidhamu na kufuata maelekezo ya benchi la ufundi. “Tunahitaji kuwa watulivu na kufuata maelekezo. Mchezo wa mtoano unahitaji umakini mkubwa kwa sababu kosa moja linaweza kubadilisha historia,” amesema.
Okello pia ameonya dhidi ya kuwadharau wapinzani wao, akibainisha kuwa heshima ni jambo muhimu katika soka. “Wapinzani wetu hawana cha kupoteza na sisi tukipoteza itakuwa habari kubwa. Ni lazima tuwabebe kwa uzito ule ule tunaotumia dhidi ya timu za ligi kuu ili kuonyesha utofauti wetu,” amesema, huku akiwataka mashabiki wa Yanga SC kujitokeza kwa wingi kutoa sapoti.

