AZIZ KI Avaa Kininja Uwanja wa Ndege, Leo Kitaeleweka, Mchezo Ulikuwa Hivi

TAARIFA ya Furaha kwa mashabiki wa Yanga ni kwamba hatimaye kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Stephen Aziz KI, amewasili nchini huku akitolewa Uwanja wa Ndege kininja. Jisajili hapa kuwa wa kwanza kushinda Mamilioni ya Meridianbet kila siku.

Aziz Ki, amewasili nchini alfajiri ya leo Julai 10, 2024 akitokea mapumzikoni kwao Burkina Faso kwa Ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia lakini akatoka kimkakati uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere terminal 3.

Alichofanya Stephen Azizi Ki, kwanza akamtanguliza mfanyakazi mmoja wa Uwanja wa Ndege mbele na mabegi yake makubwa sita aliyotua nayo.

Michezo ya Kasino na Sloti ni machimbo yanayotoa pesa kirahisi. Cheza kasino hapa.

Hatua ya pili ikawa Afisa mmoja wa Yanga Godlisten Anderson ‘Chicharito’ aliyekuja kumpokea uwanjani hapo kumpenyezea kofia maarufu kwa jina la kepu, ambayo kiungo huyo ilipomfikia akatoka akiwa ameishusha kijanja mithili ya mtu asiyetaka kujulikana.

Rais wa Yanga, Mhandishi Hersi Said amesema hadi sasa kiungo wa klabu hiyo, Stephen Aziz Ki hajasaini mkataba mpya na kwamba mazungumzo yanaendelea na anaamini kwamba watafikia mwafaka.

Injinia Hersi amesema hayo akifanya mahojiano nchini Afrika Kusini ambapo amekiri kuwa kuna klabu nyingi zinataka kumsajili nyota huyo na kwamba itakuwa ni huzuni kwao kumpoteza raia huyo wa Burkina Faso kwani bado wanahitaji huduma yake.

“Mazungumzo yanaendelea, kuna uwezekano mkubwa wa yeye kubaki [Yanga] lakini hatujafikia mwafaka,” amesema Injinia Hersi akiongeza kuwa Aziz Ki “anataka kubaki Yanga lakini mpira ni biashara siku hizi, hivyo anaweza akatamani kubaki lakini masuala ya kifedha yakamshawishi vinginevyo.”

Amesema kuwa alipomsajili Stephen Aziz Ki miaka miwili iliyopita alimweleza malengo yake ya kuiinua klabu hiyo, na kwamba nyota hiyo ni sehemu muhimu ya mageuzi ambayo yanaendelea ndani ya Jangwani.

Kasino ya Mtandaoni usipange kuacha kucheza, Meridianbet wameakuandalia Maokoto na bonasi za kasino kibao.

Acha ujumbe