AZIZ KI KUREJEA LEO KUSAINI MKATABA MPYA

Kiungo wa Ushambuliaji wa Klabu ya Yanga na raia wa Burkina Faso ambaye ni Mfungaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC) Msimu uliopita, Stephane Aziz ki anatarajiwa kuwasili nchini Tanzania leo.

Aziz Ki anarejea Tanzania na anakuja kuanza kuutumikia Mkataba wake Mpya ambao atausaini kabla ya kuingia kambini kuungana na wenzake.

Hatua hiyo inakuja baada ya Uongozi kumalizana naye kwenye kile ambacho alikuwa anakihitaji ikiwemo kumboreshea maslahi.

Acha ujumbe